Thursday, April 2, 2015

JINSI SHETANI ANAVOTUVAMIA WAKRISTU

Black Christian Dating

Hili nisomo kama yalivyo masomo mengine,liweze kukusaidia katika vita vya kiroho,kwani siku ile tu uliyomkiri Yesu kuwa bwana na mwokozi wako tayari ulitangaza uadui na shetanitabia ya adui haishi kukutafuta akuangamize.Tuone basi nijinsi gani shetani hutuvamia wakristo.

1. Shetani anachochea tamaa zetu za mwili ndani yetu kwa njia ya vitu vilivyo karibu nasi,na akijua wazi vitu hivyo nihatari kwa imani yetu kama wakristo.
2. Shetani anajaribu kutudanganya na uongo wa hekima ya kidunia kwa njia ya dunia kisicho karibu nasi.(kitu kisicho rahisi kukipata)
3. Anatumia yesu wa uongo,injili ya uongo na wakristo wa uongo (manabii wa uongo)
4. Shetani anaweza kutuvamia au wale tuwapendao kimwili yaani katika ugonjwa,uhalifu,mateso nk

   Jinsi gani sisi kusimama imara dhidi ya mashambulizi haya?
1. shetani hatujazi mawazo akilini mwetu moja kwa moja bali hutumia maneno ya uongo,shetani anaeneza uongo juu ya Mungu na anatujaza tamaa za mwili na ndio sababu wakati unatenda zambi ni wewe peke ako upo,nimwili wako ndio watenda zambi ndio sababu mwili pia hupata mateso.waefeso 6:11
2.Mkakati wa Shetani katika vita ni udanganyifu,hivyo tushinde udanganyifu kwa nguvu zote tukitumia sara na matendo mema.yohana 8:44 na mwanzo 3:1-6
3. Uasherati, yaani, shughuli za ngono nje ya ndoa
4. ubinafsi
5. ulevi uharibifu
6. Kiburi cha uzima,mafanikio kama vile pesa.

*tutakuwa pamoja katika makala nyingine jinsi ya kusimama imara kama mristo.

Ushuhuda: Mganga Asha akabidhi Mkoba wake Kanisani



Huyu siyo mwingine, bali ni Asha Mohammedi kutoka kijiji cha Kipera (Mzumbe - Morogoro).


Kwa nini afanye hivyo? Kipi kilimsibu? Fuatilia Ushuhuda huu wa ajabu,  kweli na wa kusisimua.


Asha Mohamed (36) Alipatwa na matatizo ya magonjwa kwa muda mrefu. Alikuwa na kazi ya hotelini, na kila akienda kazini, mambo yake hayaendi kama alivyotarajia. Ilifikia kipindi fulani boss wake akamfukuza kazi. Ndiposa alianza biashara ya kuuza kuku sokoni Buguruni Dar es Salaam. Biashara ilikuwa nzuri sana ila mwishowe kila akihesabu fedha yake anapata pungufu. Nyakati nyingine akajikuta hata mtaji wake unazidi kupungua siku hadi siku na kuku wa biashara akiwa nao, mathalani 300 hivi, wanaokufa ni zaidi ya 30. Kipindi hiki alikuwa na mume Muislamu baada ya kuachana na mumewe Mkristo, ambaye kwa maelezo yake walipendana sana ila ndugu zake Asha walilazimisha wawili hawa waachane ili aolewe na Muislam mwenzake.
Kwani ilikuwa je hata mara hii aolewe na Muislamu? Asha anadokeza kuwa alifunga ndoa mwaka 2010, na hakujua ndoa hii ilianza je!!. Anasema Majini ndiyo yalimuotesha ndotoni usiku juu  ya mume huyu mpya wa kiislamu atakayekuja kumuoa. Alirudi kwake nyumbani mara tu baada ya kupigiwa simu na kijana ambaye wala hakutarajia kuolewa naye. Walifanya taratibu zote na wakaoana.  Ingawa mume huyu naye ni wa pale kijijini Kipera, lakini Asha anasema alimpa sharti huyu mwanaume, kuwa hajazoea maisha ya kijijini hivyo baada ya ndoa itabidi warudi Dar es Salaam. Hata hivyo, ugomvi haukupungua nyumbani. Tokea akiwa na mwezi mmoja tu wa ujauzito, Asha alianza kuumwa  mfululizo na madaktari wasiweze kumpatia tiba. Siku zilipokaribia kujifungua, Asha alipelekwa Zahanati ya Mzumbe, lakini madaktari wakasema apelekwe Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwani wataalamu wa hali kama ile watapatikana. Hata hivyo,  alipofikishwa Hospitali Kuu ya Morogoro, madaktari bila hata kumpima, walimuingiza Chumba cha Upasuaji,  na wakamtoa mtoto. Bahati mbaya, mtoto yule aliishi muda mfupi tu,  na siku ya 3 kichanga hiki kikafariki dunia. Matatizo ya magonjwa kwa Asha yakaendelea kushika kasi.


Ndipo wakahamia TIBA MBADALA!!! Mmoja wa waganga wa kienyeji alikowahi kupelekwa kutibiwa alimwambia Asha kuwa anapaswa akakabidhiwe MKOBA. Mama mzazi naye alimshawishi Asha apokee huo mkoba ili kuumwa kwake kuishe. Akakubali kupokea mkoba huo Oktoba 2011. 

Je kuna gharama yoyote kupata mkoba kama huu? Ndiyo. Asha anasema ni gharama sana kupata mkoba,  na alilipia Sh. 150,000 (Laki na Hamsini elfu) kupatiwa mkoba huu. Mganga wa kienyeji aitwae Sefu anayeishi Kipera (hadi sasa) ndiye alimkabidhi mkoba huo.  Kazi ilianza rasmi ya kuagua.  Akawa anatibia wateja wengine wenye shida mbalimbali,  ikiwemo maradhi na kusuluhisha ndoa zao lakini yeye binafsi akabakia kuwa ni mgonjwa na hawezi kujitibia. Ndiyo maana, pamoja na uganga wake, Asha alikuwa akienda kwa waganga wengine maeneo mbali mbali Tanzania  kama Tanga, Sumbawanga n.k ili kujipatia tiba bila mafanikio.

Jumanne wiki jana (15/07/201) Asha alipelekwa kwa mganga mwingine, na ambaye ndiye wa mwisho kabla ya kuokoka na kuachana na ushirikina. Mganga huyu alimchinja jogoo na kumpika, kisha ile sahani yenye nyama za hiki chakula ikawekwa juu ya kichwa cha mama huyu. Baadae watoto 7 walitafutwa hapo mtaani wakaitwa ili kula hiki chakula juu ya kichwa cha Asha. Watoto hawa walipewa masharti kuwa, ni marufuku kutafuna mifupa ya huyo jogoo. Mumewe alipewa masalia ya mifupa ile na kwa kuwa Morogoro  hakuna bahari, aliagizwa akaitupe kwenye mto mmoja hivi huko Mlali ambao maji yake yametulia na hayaendi haraka. Alifanya hivyo, lakini pamoja na hayo, waliporudi nyumbani matatizo ya Asha yalimrudia upya. 

Yapi madhara ya ule mkoba? Kwa mujibu wa Asha, Mkoba ule haukumruhusu aoge, wala kufua,  wala kupiga mswaki. Siku nzima alikuwa ni mama wa kulala kitandani tu. Mumewe ndiye alikuwa akifanya kazi za kufua nguo, kupika chakula n.k. kiasi kwamba ndugu za mwanaume walianza kufikiria kuwa mama huyu  amemwekea 'limbwata" mume wake. Hata wateja wake walianza kupungua na akimpata mteja wa sh. 5,000 ilikuwa ni bahati. 
Picha 2: Baadhi ya Shehena ya vifaa vya uganga (Mkoba) ambao Asha
alikabidhi kanisani kabla ya kuteketezwa kwa moto Ijumaa 18/07/2014
chanzo: email kutoka kwa grace fella,ufufuo a uzima morogoro

Sunday, March 15, 2015

USHUHUDA KUTOKA KWA MAMA MAHMUD KOMANYI

Kutoka Newala,Mtwara
Ilikuwa ni tarehe 11 mwezi wa 2 asubuhi, kama kawaida ya waafrika wengi kula yetu kubwa inatoka shambani,nilijihimu kwenda bondeni kuchuma mboga na kuokota kuni,nikiwa na toka nyumbani nilirudishia mlango ili usijibamize ukamwamsha mme wangu na mtoto wangu wa kiume anaeitwa Mahmud.
Nilifika bondeni baada ya dakika kama ishirini hivi lakini ilikuwa bado mapema sana,wakati nachuma  mboga nikaona begi la wastani ambalo limefichwa bustanini kwangu,nilishtuka sana nikatazama vizuri begi lile nikaona lina damu juu ikiwa haija kauka vizuri,nikapata wazo yawezekana kuna wezi wamempora mtu begi lile kisha wakiwa wanakimbizwa wakaona niheri walifiche pale ili walifate baada ya muda,niliona nivema nilifungue nione kuna nini mle ndani,looh!nilikuta kuna fedha mabunda mawili,paspoti ya kusafilia na biblia kubwa,nilitazama pande zote sikuona mtu anaye nitazama,basi nikalifunga begi vizuri nikatoa kanga nikaliviringisha begi kisha nikatimua mbio kwenda nyumbani kwa mme wangu.
Mume wangu alishangaa tukaona inshallah mwenyazi Mungu ametujalia neema ya fedha zile ili tutatue matatizo yetu,baada ya dakika ka ishirini hivi walivamia vijana watatu mmoja akiwa anamajeraha mengi usoni na misuri iliyojaa,akatoa panga akanisogelea nakunambia kwa sauti kali “begi lipo wapi”niliogopa muda uwo wale vijana wawili wamemkaba mme wangu,nikaona sina budi kusema uwongo nikamwambia lipo chini ya kitanda,akasema “litoe weka juu ya kitanda”nikalitoa,akalichukua akafungua nakutazama ndani,akatoa yale mabunda mawili ya fedha kisha akatoa paspoti yakusafilia akaichana,na baadae biblia akaigeuza akaitazama kisha akaitupia chini ya kitanda.wakatufunga kamba mlendani kisha wakatoweka.
Ilipita siku mbili baada ya tukio hilo kutokea nikiwa sijakumbuka kuitoa biblia ile chini ya kitanda na ukizingatia sio kitabu cha imani  yangu. Tukiwa tumelala usiku mume wangu alikuwa anakoroma sana kisha anatoa mapovu meupe mdomoni yenye harufu mbaya sana,nikaamka nikawasha kibatali ili nimtazame vizuri,alikuwa akijipiga piga huku analalamika anasema “mnanionea bure,sijui chochote”nikapiga kelele ili niombe msaada lakini gafla nikapigwa nikapigwa na kitu kizito kichwani nikazimia.nimekuja kuzinduka asubuhi namuona baba watoto wangu,baba mkwe,mama mkwe,na wazee watatu wakiwa wamekaa chini mle chumbani wamechoka sana tena uchi kabisa,nilipigwa na butwaa ikabidi niombe msaada.alikuja jirani yetu ambaye nimganga wa kienyeji iliawasaidie maana walikuwa hawaongei wala hawatikisiki,alipo fika akawatazama akaangalia chumba chote kisha akasema ndugu zako wamechoka sana kunakitu walichokuwa wanapigana nacho kimewazidi nguvu,niwewe umechanjwa,nilishangaa sana nikamwambia mganga tangu lini mimi najihusihsa na ayo mambo,kwanza kabisa nipo kwenye ndoa yangu tangu mwaka 1997 lakini sikuwahi kujua kama mume wangu na wazazi wake niwashirikina,alinitazama kwa jicho kali kisha akafumba macho kama dakika mbili  hivi,gafla akaenda kwenye kitanda akakibinua kwa nguvu arafu akarudi nyuma,akanitazama nakusema “nini hiki,unabisha huna uchawi nini hiki nakuuliza!” nilishangaa sana,nikaenda ilipokuwa biblia nikaiokota nikaenda nayo sebureni,nilipo toka tu mme wangu na wazazi wake ufahamu ukawarudia.

Tangu siku hiyo mume wangu anaona hay asana,hana amani,nilistahajabu sana juu ya jambo lile niliona vyema kuitunza biblia hile na kuisoma kila siku, niliona nivyema nivunje ukimya nizungumze na mme wangu kwamba asijali nimemsamehe na siwezi kumkimbia baada ya kumgundua,nilistaajabu alipo niambia kwamba,tangu siku ile wazazi wake hawamtembezi tena usiku wala kumtuma maana humfanyisha kazi zakishirikina bila ridhaa yake,hivyo anatamani kuwa anasoma biblia kila siku,na angependa familia nzima tubatizwe,ilikuwa nijambo lakushangaza sana na hasa nikitafakari jinsi ile biblia ilivotufikia nyumbani kwetu,basi sichoki kusema ASANTE YESU. 

Saturday, March 14, 2015

Tabia za mume aliye badilika


Katika vitu ambavyo Mungu ametupendelea ni UTASHI,hivyo basi tunapaswa kutambua dalili zote zile katika maisha ziwe nzuri au mbaya. katika makosa makubwa ambayo sisi kama wakristu tunayafanya nipale ambapo tunachagua wenza wetu kwa kutumia milango mitano tu yafahamu tuliyonayo bila kumuhusisha roho mtakatifu.kupata mweza kanisani au wakati wa kwaya pekee haitoshi kuamini kwamba umepata kilicho bora,yawezekana akawa muumuni mzuri kipindi hiko ili aweze kukamilisha kazi yake ya ulaghai.

Kwa sababu hiyo nawaambia, chochote mtakachoomba katika sala,mtapata Marko 11:24
basi endapo utaziona dalili hizi mwambie Mungu alete amani katikati yenu

1. wewe daima nitatizo,kila kitu anakulaumu wewe,
2. haoni mema unayo mtendea,yote kwake uyafanyayo nisawa na bure
3. kamwe hataki kubadilika, umemsihi sana lakini amekuwa mgumu hii inaashiria mume wako upendo wake kwako umepungua.
4. hakuali kama zamani,kwa sasa hata kadi tu ya kristmasi anasahau kukuletea.
5.  hapendi kukaa na wewe kwamuda mrefu,anakukwepa.
Usisite kuwa shirikisha walezi wako wa kiroho pamoa na ndugu wakaribu wenye hekima,uu ya mabadiliko hayo ya mumeo lakini kubwa zaidi tafakali mwenendo wako na wapi ulianguka yawezekana tabia yako yanyuma au mwenendo wako wasasa unamfanya mumeo abadilike,Lakini kubwa zaidi ni kumshirikisha MUNGU...Waebrania 11: 1

Friday, March 13, 2015

Misingi ya ukombozi


Kujua wewe ni nani katika Kristo
 Moja, tunapaswa kuelewa kile ambacho Kristo amefanya kwa ajili yetu, na ambapo sisi tunasimama. Kama sisi ni waumini katika Kristo Yesu, basi nasisi tumeketi pamoja naye katika maeneo ya mbinguni (Efe 2: 6). Hii inasababisha sisi kuwa juu juu ya malaika (na mapepo) katika ulimwengu, na haki yetu uko juu nikuwa karibu na Yesu! Hivyo badala ya kuangaliwa na mapepo, basi sasa tunaweza kuangalia chini hadi juu yao, ambapo inafakunya  wewe ni kupigana vita vya kiroho.

Kuelewa mamlaka yetu juu ya adui
Ni muhimu pia kuelewa mamlaka tuliyopewa juu ya nguvu zote za yule adui.Tumepewa mamlaka juu ya nguvu zote za yule adui (Luka 10:19 & Mark 16: 15-18).Naamini na mamlaka, tumepewa wajibu.Siamini kama sisi ni kuomba na kumuuliza Bwana pepo kutoka, naamini kwamba ni jambo ambalo sisi wenyewe ni kufanya.Najua linapokuja kufunga na kufungua, kuna mahali pa katika NT kwamba inatuambia kuomba na kumuomba Mungu kumfunga shetani.Lakini haina kusema kwamba WEWE ni kuwafunga, na WEWE ni huru. Mathayo 16:19, "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni:na lo lote * Na wewe nawe utakalolifunga duniani, kitafungwa pia mbinguni;na lo lote ndiwe utakuwa huru duniani kitafunguliwa mbinguni. "Yesu alitupa funguo, lakini ni juu yetu kuzitumia!.
Haki kisheria
Kuna seti ya 'sheria' zinazotumika katika ulimwengu wa kiroho. Wakati sisi kukiuka sheria hizi, ni kufungua sisi juu ya adui.Agano la Kale ni sehemu kubwa ya kujifunza kuhusu sheria hizi. Kwa mfano, kama mtu kulala na mke wa kaka yake, hii inaweza kuleta laana juu ya watu hao(Sheria 20:21).Kujihusisha na uchawi nisawa na dhambi ya ngono.Wakati mwingine mababu zetu hawana msaada katika mambo yoyote (Kutoka 20: 5). Baadhi ya milango mingine ya kawaida ni pamoja na kuwa mchungu na asiyesamehe (Mathayo 18: 23-35) au watumia vitu (kama pete uchawi au sanamu).

Ili kuiweka kwa kifupi:

Ni muhimu kujua 'haki' yetu (yale Yesu alifanya kwa ajili yetu, mamlaka yetu, nk). Ni muhimu pia kujua sisi ni nani katika Kristo. Moja ya hatua muhimu sana katika ukombozi, ni kufikiri nini alifungua mlango na adui (kisheria haki), na kuziba milango ile. Basi ni jambo la kutumia mamlaka yetu ya kuwafukuza pepo.

Mpenzi anaye kufaa


Upendo katika husiano unaweza kuongeza mambo mengi ya maisha yako, yaani hisia zako na akili ni vizuri zikadumisha furaha kwa ujumla.Kwa wengi wetu, ingawa, kutafuta mtu wa kushiriki maisha yetu  inaweza kuonekana kama ni kazi na haiwezekani.
Lakini si kukata tamaa, hata kama una historia ya mahusiano ambayo si imara au kama wewe umeisha wahi kuumizwa, bado unaweza kujifunza jinsi ya kutafuta kudumu katika  upendo.

Warumi 12: 9, Upendo ni lazima uwe wa dhati. Chukia maovu, bali shikamana na yaliyo mema.

Hatua ya kwanza ya kutafuta mpenzi mzuri ni kutofautisha kati ya nini unataka na nini unahitaji katika mpenzi. Ningependa katika mpenzi,iwe ni pamoja na kazi, akili, na sifa za kimwili kama vile urefu, uzito, na rangi ya nywele. Hata kama sifa fulani inaweza kuonekana kuwa muhimu sana kwa mara ya kwanza, baada ya muda utasikia  kwamba kuna kasolo katika uchaguzi wako. Kwa mfano, inaweza kuwa muhimu zaidi, au angalau kama  ukipata mtu ambaye ni:

1.mdadisi na nimwelewa
2.mwenye kujali nasio kutazama uzuri wa sura au umbo
3.mwenye hisia juu yako na sio mpenda ngono
4.mtu mwenye maadili safi nasio utajili au ukabila
5.mcha Mungu na ni mkweli hata anapokosea hasiti kukili kosa.
Soma zaidi Waefeso 4: 2