Ilikuwa ni tarehe 11 mwezi wa 2 asubuhi, kama kawaida ya
waafrika wengi kula yetu kubwa inatoka shambani,nilijihimu kwenda bondeni
kuchuma mboga na kuokota kuni,nikiwa na toka nyumbani nilirudishia mlango ili
usijibamize ukamwamsha mme wangu na mtoto wangu wa kiume anaeitwa Mahmud.
Nilifika bondeni baada ya dakika kama ishirini hivi lakini
ilikuwa bado mapema sana,wakati nachuma
mboga nikaona begi la wastani ambalo limefichwa bustanini
kwangu,nilishtuka sana nikatazama vizuri begi lile nikaona lina damu juu ikiwa
haija kauka vizuri,nikapata wazo yawezekana kuna wezi wamempora mtu begi lile
kisha wakiwa wanakimbizwa wakaona niheri walifiche pale ili walifate baada ya
muda,niliona nivema nilifungue nione kuna nini mle ndani,looh!nilikuta kuna
fedha mabunda mawili,paspoti ya kusafilia na biblia kubwa,nilitazama pande zote
sikuona mtu anaye nitazama,basi nikalifunga begi vizuri nikatoa kanga
nikaliviringisha begi kisha nikatimua mbio kwenda nyumbani kwa mme wangu.
Mume wangu alishangaa tukaona inshallah mwenyazi Mungu
ametujalia neema ya fedha zile ili tutatue matatizo yetu,baada ya dakika ka ishirini
hivi walivamia vijana watatu mmoja akiwa anamajeraha mengi usoni na misuri
iliyojaa,akatoa panga akanisogelea nakunambia kwa sauti kali “begi lipo wapi”niliogopa
muda uwo wale vijana wawili wamemkaba mme wangu,nikaona sina budi kusema uwongo
nikamwambia lipo chini ya kitanda,akasema “litoe weka juu ya kitanda”nikalitoa,akalichukua
akafungua nakutazama ndani,akatoa yale mabunda mawili ya fedha kisha akatoa
paspoti yakusafilia akaichana,na baadae biblia akaigeuza akaitazama kisha
akaitupia chini ya kitanda.wakatufunga kamba mlendani kisha wakatoweka.
Ilipita siku mbili baada ya tukio hilo kutokea nikiwa
sijakumbuka kuitoa biblia ile chini ya kitanda na ukizingatia sio kitabu cha
imani yangu. Tukiwa tumelala usiku mume
wangu alikuwa anakoroma sana kisha anatoa mapovu meupe mdomoni yenye harufu
mbaya sana,nikaamka nikawasha kibatali ili nimtazame vizuri,alikuwa akijipiga
piga huku analalamika anasema “mnanionea bure,sijui chochote”nikapiga kelele
ili niombe msaada lakini gafla nikapigwa nikapigwa na kitu kizito kichwani
nikazimia.nimekuja kuzinduka asubuhi namuona baba watoto wangu,baba mkwe,mama
mkwe,na wazee watatu wakiwa wamekaa chini mle chumbani wamechoka sana tena uchi
kabisa,nilipigwa na butwaa ikabidi niombe msaada.alikuja jirani yetu ambaye
nimganga wa kienyeji iliawasaidie maana walikuwa hawaongei wala
hawatikisiki,alipo fika akawatazama akaangalia chumba chote kisha akasema ndugu
zako wamechoka sana kunakitu walichokuwa wanapigana nacho kimewazidi
nguvu,niwewe umechanjwa,nilishangaa sana nikamwambia mganga tangu lini mimi
najihusihsa na ayo mambo,kwanza kabisa nipo kwenye ndoa yangu tangu mwaka 1997
lakini sikuwahi kujua kama mume wangu na wazazi wake niwashirikina,alinitazama
kwa jicho kali kisha akafumba macho kama dakika mbili hivi,gafla akaenda kwenye kitanda akakibinua
kwa nguvu arafu akarudi nyuma,akanitazama nakusema “nini hiki,unabisha huna
uchawi nini hiki nakuuliza!” nilishangaa sana,nikaenda ilipokuwa biblia
nikaiokota nikaenda nayo sebureni,nilipo toka tu mme wangu na wazazi wake
ufahamu ukawarudia.
Tangu siku hiyo mume wangu anaona hay asana,hana amani,nilistahajabu
sana juu ya jambo lile niliona vyema kuitunza biblia hile na kuisoma kila siku,
niliona nivyema nivunje ukimya nizungumze na mme wangu kwamba asijali
nimemsamehe na siwezi kumkimbia baada ya kumgundua,nilistaajabu alipo niambia
kwamba,tangu siku ile wazazi wake hawamtembezi tena usiku wala kumtuma maana
humfanyisha kazi zakishirikina bila ridhaa yake,hivyo anatamani kuwa anasoma
biblia kila siku,na angependa familia nzima tubatizwe,ilikuwa nijambo
lakushangaza sana na hasa nikitafakari jinsi ile biblia ilivotufikia nyumbani
kwetu,basi sichoki kusema ASANTE YESU.
0 comments:
Post a Comment